App mpya ya Kisukari.com itapatikana hivi karibuni ili kukusaidia kudhibiti na kufuatilia hali yako ya kisukari kwa urahisi.

Kwa usajili wa mapema tafadhali jaza fomu iliyo hapa chini.

Itapatikana

Kudhibiti kisukari kunaweza kuwa changamoto, lakini hauko peke yako. Usijali Programu yetu imeundwa KWA AJILI YAKO.

Fuatilia viwango vya sukari kwenye damu, vipimo vya presha na mapigo ya moyo.

Tutakusaidia kufuatilia matumizi ya dawa na sindano za insulini pamoja na kukumbusha kuzingatia matibabu.

App yetu itakusaidia kufuatilia na kukumbusha mahudhurio yako ya kliniki.

Dhibiti kisukari kwa lishe bora na mazoezi.

Pata taarifa kuhusu viwango vya virutubisho katika chakula chako na jinsi inavyoathiri viwango vyako vya sukari. Hii itakusaidia kufanya uchaguzi bora wa chakula kwa afya bora.

Fanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku kwa kutumia mipango ya mazoezi iliyoundwa na wataalamu. Pata ushauri kuhusu aina bora za mazoezi zinazosaidia kudhibiti viwango vya sukari na kuboresha afya yako kwa ujumla.

Pata ripoti za kibinafsi na uchambuzi wa kina kutoka kwa wataalamu wetu.

App yetu inakupa ripoti za kibinafsi na uchambuzi wa kina kutoka kwa madaktari wenye uzoefu ili kukusaidia kuelewa afya yako vizuri zaidi.

Jiunge na jamii yetu mtandaoni.

Kisukari.com sio tu kuhusu kufuatilia afya yako; ni pia kuhusu kujenga jamii yenye nguvu na inayosaidiana.

Jamii yetu ni mahali salama na rafiki ambapo unaweza kuuliza maswali, kutoa ushauri, na kupata msaada kutoka kwa watu wanaoelewa kile unachopitia. Ukiwa na Kisukari.com, hauko peke yako; una jamii nzima inayokusaidia.